HISTORIA YA "WASUKUMA"
Jina la Wasukuma limetokana na neno SUKUMA(KASIKAZINI).
Hivyo Msukuma ni mtu wa Kasikazini
lakini Wasukuma haimaanishi tu watu wa kaskazini bali wanajumuishwa pia watu wa
1.Mashariki(Bhanakiya:Ntuzu):Mkoa wa Simiyu.
2.Kusini(Wadakama,hawa wanaweza kuwa Shinyanga ama Tabora kutegemeana upo wapi).
Msukuma wa Mwanza yeye ndio anaona yupo kaskazini hasa kuliko wote kwa hiyo akiwaita watu wa Shinyanga ni wa Kusini(Wadakama) hawezi kuwa amekosea.Japo ukiwa Shinyanga napo utawasikia watu wa Shinyanga wakisema wao wapo kaskazini hivyo ni wasukuma na kusini yao ndio kuna wadakama(Mkoa wa Tabora ndio upo kusini). Inajulikana zaidi kuwa Wenyeji wa Tabora ni Wanyamwezi.Usukumani hakuna kabila la Wanyamwezi bali wanaitwa Wadakama. Japo ukifika Tabora wilaya ya Sikonge na Urambo hasa yenye Wanyamwezi huku wilaya zingine zikiwa kwa kiasi kikubwa zimekaliwa na wasukuma waliotokea Shinyanga na Mwanza miaka mingi iliyopita.
3.Magharibi(Bhanang'weli). Huku utakutana na Wasumva/Wasumbwa. Hawa ndio wanachukua sehemu ya watu wa Magharibi.
Wasumbwa kama ilivyo kwa Wanyamwezi wao wanaonekana kama si sehemu ya Wasukuma lakini ni sehemu ya wasukuma na karibu kila kitu kinafanana kuanzia lugha,mila na desturi na utamaduni wao.
4.Kaskazini(Wasukuma).
Kwa hiyo Wasukuma wamegawanyika katika pande kuu nne za dunia na jina la pande moja ya Kaskazini ndio lililochukua nafasi ya pande zingine zote.
Kabila la wasukuma linapatikana mikoa mitano Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu na Tabora.
Japo wanyamwezi asili kabisa ni wachache na wanachukua wilaya ya Sikonge na Mirambo, wilaya zingine zikikaliwa na Wasukuma kuanzia Igunga na Nzega ama mchanganyiko kama Uyui.
hii ni mikoa asili ambayo wasukuma wanatokea.
Wasukuma wengi pia wanapatikana katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Morogoro.Ambapo wamehamia huko kwa ajili ya kufata kilimo na malisho ya mifugo.
Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi nchini Tanzania likifuatiwa na Kabila la Wahaya na baadae Wachagga
Hata mimi Kaka Emanuel Msoka Admin wa Online News Tz page inayoongoza kwa simulizi kali za kusisimua, elimu mikasa ya kusisimua na habari za uhakika nina rafiki zangu wengi sana wasukuma, pia viongozi wengi katika nchi hii wanaosifika kwa utendaji wa kiwango cha juu akiwemo mheshimiwa Rais na wakuu mbalimbali wengi ni wasukuma.
MILA NA DESTURI.
Kama ilivyo makabila mengine ya Kiafrika wasukuma wana mila zao na tamaduni zao.Mila za wasukuma zimegawanyika sehemu mbili.
1.Mila za koo ama familia.Hizi hazifanani kabisa kati ya koo na koo.
2.Mila za jumuiya. Hizi zinafana na zinajulikana kwa wanajumuiya/wanachama bila kujali ni wasukuma wa Mwanza,Simiyu(Ntuzu),Tabora(Wanyamwezi),Shinyanga ama wamagharibi(bhanang'weli=wasumbwa).
Jumuiya za mila zipo mbili.
(i)Bhakango,hawa wanafanya kitu kinaitwa bhukango.
Mila hizi zinahusu wazazi na watoto wa aina:-
kwanza watoto mapacha.
Ukizaa watoto mapacha ni mkosi hivyo lazima ufanye bhukango kuondoa mikosi.wa pili ni watoto waliozaliwa wametanguliza miguu(Kashinje/kashindye).
Mtoto akitanguliza miguu kwa maana ya kuzaliwa kinyumenyume huo ni mkosi na lazima ufanye bhukango.Wazazi wa mtoto ama watoto mapacha hupelekwa kufanyiwa matambiko maeneo kama mtoni na huko wao watakuwa uchi kabisa huku wakifanyiwa hayo matambiko na wanajumuiya wenzao
Kwa wasioshuhudia siku ukibahatika
Labda mpaka upate mikosi ama matatizo na uelekezwe na wataalamu wa mila kuwa hao mapacha ama huyo kashinje ndio tatizo basi utalazimika na wewe kuwa mwanachama/mwanajumuiya.
Ili uwe mwanachama sharti uzae mapacha,kashinje,ama wewe ni pacha,ama waliokutangulia ni mapacha mfano ni Shija ambaye huzaliwa baada ya mapacha naye ana sifa ya kuwa mkango.
(ii)Bhasweji, hili ni kundi la pili la wanamila wa kisukuma.
Kundi hili ndio hushughulika na matambiko ya kila aina iwe ni kuondoa mikosi,neema n.k
Hapa si lazima uwe mwanachama wa moja kwa moja kufanya matambiko haya. Ukipata mikosi,laana nk na njia pekee ni ya kuondoa mikosi hiyo ni matambiko basi hawa mabwana watakuja kukufanyia hata kama si mwanachama.Ila matambiko na ngoma watacheza na kufanyia kwako.
Chakula chao hawali kitu kingine zaidi nyama. Fanya ufanyavyo nyama isikosekane. Kama unapika ugali mboga ni nyama. Kama wali mboga ni nyama.Na wanatabia huwa hawaondoki na wanaweza kukaa kwako hata mwezi wanatambika tu.Usipopika nyama siku hiyohiyo wanaondoka.
WASUKUMA NA NDOA.
Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitaala(mke zaidi ya mmoja).
Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahali ya ng'ombe kati ya ng'ombe 7 mpaka 20. hii ni kawaida.lakini mahali inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 kutegemeana na mazingira ya anaeolewa na muoaji.Lakini kubwa kuliko yote ni uzuri na tabia nzuri ya mwanamke.
wasukuma huzaa watoto wengi. Kwa wastani watoto kati ya 6 mpaka 8 ama zaidi na hao ni wa mama mmoja
WASUKUMA NA WANAWAKE WEUPE.
Ni kweli wasukuma wanapenda wanawake weupe ila weupe natural.
Lakini hili la wanawake weupe si la Wasukuma peke yake bali ukweli ni asimilia kubwa ya wanaume wa makabila yote wanapenda wanawake weupe ila wasukuma ndo wanasingiziwa zaidi utazani wengine hawawapendi wanawake weupe
Wasukuma wamejaliwa mabinti wazuri sana wenye maumbo mazuri, warefu wenye nyama kiasi halafu wenye black beauty yaani rangi iliyo katikati ya nyeupe na nyeusi, uzuri wao mabinti wengi wa kisukuma wanajikubali hivyo sio watumiaji wa vipodozi vikali ndio maana ni ngumu mno kumkuta binti wa kisukuma amejichubua.
NGOMA.
Wasukuma wana aina ya ngoma za burudani zaidi ya 15.
USHAMBA WA WASUKUMA.
Kuna mambo mawili hapa.
1.Wasukuma wana watani wao.
Ushamba wa msukuma umejengwa juu ya watani wa msukuma. Ambapo ni kawaida sana kwa makabila watani wa msukuma kumtania msukuma japo utani unaweza kuwa unabeba sehemu ya ukweli kwa anaetaniwa ila haimaanishi ndo wasukuma wote wapo hivyo.
Mzee mmoja wa kisukuma aliwahi kuniambia maneno haya,
Nje ya makabila watani wa msukuma hata makabila mengine yanatania wasukuma hasa kutokana na ukweli kuwa msukuma kwa kiasi kikubwa hanaga tatizo na jamii yoyote ukiacha wamasai waliokuwa wanatuibia ng'ombe zetu enzi na enzi japo hili sasa ni kama halipo.
2.Maisha ya kijijini. Kama ilivyo makabila mengine wasukuma wengi zaidi wanaishi vijijini na maisha ya vijijini yanafanana kwa karibu makabila yote nchini. kama ni uduni wa mavazi na malazi yanafanana na watu wa vijijini katika jamii zingine,Kama ni kutoyafahamu vyema maisha ya mjini basi ni sawa na watu wa vijijini katika makabila mengine hata kwa watani zetu wagogo.kwa hiyo ieleweke kuwa kila kabila lina washamba na wasio washamba kutegemeana na aina ya ushamba na mazingira ya huyo mshamba
UNDANI WA WASUKUMA
Wasukuma ni kabila kubwa zaidi nchini Tanzania: linakadiriwa kufikia watu milioni 7, idadi inayowakilisha asilimia 16 ya wakazi wa nchi kwa ujumla.
Jina "Wasukuma" lina maana ya watu wa upande wa "kaskazini", lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano Wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira) kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili: Kiya. Hili lina maana ya mashariki ambako ni maawio ya jua. Huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani. Mfano mwingine ni upande wa "Dakama" ambapo yatambulisha kama eneo la Unyamwezi lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa "kusini". Zaidi ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila la Wanyamwezi ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma nao husema "dakama". Upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho ni "Ushashi" maana yake ni upande wa kabila la Washashi na neno hili Washashi ni mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa mara, japo pia neno hili "shahi" linamaanisha kabila la Wakurya ambalo pia mpanuko wake unakomea hapo, ambapo zaidi ya hapo eneo zima la upande huo unamaanisha upande wa kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa ni "Ngw’eli", neno hili halikupewa kabila na badala yake linawakilisha upande wa magharibi (dira), ambako ni machweo ya jua. "Wasukuma wenyewe hulirejea jina hili kama "Basuguma" kwa wingi na "Nsuguma" kwa umoja.
Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania, karibu na mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria, na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, upo pia kusini magharibi mwa mkoa wa Mkoa wa Mara, Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Shinyanga.
Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika mbuga maarufu Serengeti. Familia za Wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanywa na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo ya kabila la Wapimbwe na hivyo kufanya makazi katika eneo hili la kijiji cha Wapimbwe.
Eneo hili linakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba 910 hadi 1200.
Mwinuko wake unakadiriwa kuwa inchi 20 hadi 40 ya ujazo wa mvua kutoka Novemba hadi Machi.
Kiwango cha juu cha joto hutegemea angalau ni kutoka wakati kiwango cha chini nyakati za usiku hushuka na kufikia 15°C.
Maeneo yaliyo na madini
Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali. Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini: 1. Mwadui (Huku kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia serikali pesa za kigeni) 2. Maganzo (Vilevile eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui.)
Shughuli za kiuchumi
Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara.
Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku, mahindi, viazi, dengu na matunda (kisiwani Ukerewe)
Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo ambayo huchimbwa katika maeneo mbalimbali mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Wasukuma pia wanajihusisha sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbalimbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama mahindi na mpunga.
Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima wa mbogamboga.
Shughuli za sherehe
Wasukuma wengi katika karne ya 20 walitumia utamaduni wao zaidi katika kusherehekea matukio ya nyakati mbalimbali, kwa mfano wakati wa mavuno, unyago, ndoa, misiba n.k.
Watemi ndio walikuwa viongozi wa kabila la Wasukuma na watu walikaa kiukoo katika eneo moja.
Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia historia hii murua ya wasukuma,
Nakutakia Siku Njema

No comments